80- Kisha alete Takbiyr zilizobaki na atakase ndani yake du´aa juu ya maiti. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Umaamah iliotangulia punde kidogo. Vilevile kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mnapomswalia maiti basi mtakasieni juu yake du´aa.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud (02/68), Ibn Maajah (01/456), Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (754- Mawaarid), al-Bayhaqiy (04/40) kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah ambapo Abu Ishaaq amesema wazi kwamba amehadithia kwa Ibn Hibbaan.

[1] as-Sindiy amesema:

”Mkusudieni yeye kwa du´aa.”

al-Munaawiy amesema:

”Bi maana muombeeni kwa kumtakasia nia na kuhudhuria kwa moyo. Kwa sababu kinachokusudiwa kwa swalah hii ni msamaha na kumuombea uombezi maiti. Hakika si vyenginevo kutarajiwa kukubaliwa katika mazingira ya kujaa Ikhlaasw na kuonyesha unyonge. Kwa ajili hiyo ndio maana imewekwa katika Shari´ah katika kumswalia katika du´aa ambazo hazikuwekwa katika Shari´ah mfano wake katika kumuombea aliyehai. Ibn-ul-Qayyim amesema: ”Haya yanabatilisha maneno ya yule aliyedai kuwa maiti hanufaiki kwa maneno yoyote.”

Katika upokezi wa al-Haakim kutoka katika Hadiyth ya Abu Umaamah iliyotangulia: ”Aitakase swalah katika Takbiyr tatu.” Swalah hapa ni kwa maana ya du´aa. Hilo ni kwa dalili ya upokezi wa kwanza: “Aitakase du´aa.” Kwa sababu msingi wa maana ya swalah kilugha ni du´aa. Miongoni mwa mambo ya kushangaza ni yale yaliyotajwa katika “al-Qawl-ul-Badiy´”, uk. 152:

“Aitakase swalah.”

ambapo yeye akafasiri kwa kusema kwamba ainue sauti yake ndani ya swalah yake kwa Takbiyr tatu!

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 156
  • Imechapishwa: 02/02/2022