77. Tofauti kati ya nguzo na mambo ya wajibu ya swalah


Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ikiwa nguzo hata moja itaachwa, sawa kwa kukusudia, au kutokukusudia swalah inabatilika kwa kuiacha.

Ikiwa jambo la wajibu litaachwa kwa kukusudia, swalah yabatilika kwa kuliacha, na ikiwa litaachwa kwa kutokukusudia, itakuwa ni wajibu kuleta Sujuud ya kusahau.

MAELEZO

Hapana tofauti inapokuja katika nguzo kati ya kusahau na kukusudia. Ni lazima kuifanya. Imamu au yule anayeswali peke yake kwa mfano akiacha kusoma al-Faatihah kwa makusudi swalah yake inabatilika. Akiiacha kwa kusahau swalah yake inabatilika. Endapo ataswali ilihali ameacha nguzo basi ni lazima aifanye. Kukipita kitambo kirefu ni lazima aianze swalah mwanzo.

Kuhusu mambo ya wajibu akiyaacha kwa makusudi swalah yake inabatilika. Akiyaacha kwa kusahau atasujudu Sujuud mbili za kusahau mwishoni mwa swalah yake ambazo ataunga kwazo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 109
  • Imechapishwa: 06/07/2022