77. Mwanamke kushushwa ndani ya kaburi na asiyekuwa Mahram wake

Swali 77: Je, mtu ajitolee kushuka chini ya kaburi ikiwa aliyekufa ni mwanamke na hana walii[1]?

Jibu: Hapana neno kufanya hivo hata kama mawalii wake watakuwepo pale. Mmoja katika wasichana zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwekwa ndani ya kaburi lake na wasiokuwa Mahaarim zake licha ya yeye mwenyewe kuwepo pale (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/191).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 56
  • Imechapishwa: 01/01/2022