Swali 77: Je, mtu ajitolee kushuka chini ya kaburi ikiwa aliyekufa ni mwanamke na hana walii[1]?
Jibu: Hapana neno kufanya hivo hata kama mawalii wake watakuwepo pale. Mmoja katika wasichana zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwekwa ndani ya kaburi lake na wasiokuwa Mahaarim zake licha ya yeye mwenyewe kuwepo pale (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/191).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 56
- Imechapishwa: 01/01/2022