77. Muislamu ambaye hakutubia juu ya madhambi yake


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Amepuuzilia mbali madhambi yao makubwa kutokana na kutubia kwao na akawasamehe madhambi yao madogo kwa sababu ya kujiepusha kwao na madhambi makubwa. Amefanya ambaye hakutubu kwa madhambi makubwa anaingia chini ya utashi Wake:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[1]

MAELEZO

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anawasamehe wale anaowataka:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا

“Endapo mtajiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa, basi Tutakufutieni madhambi yenu madogo na tutakuingizeni katika mahali patukufu.”[2]

Kuyaepuka madhambi makubwa ni njia moja wapo ya kusamehewa madhambi makubwa. Madhambi madogo yanasamehewa pia kwa kutubia. Mtenda dhambi akifa hali ya kuwa bado yuko katika hali hiyo na akafa pasi na kutubia kwa madhambi ambayo yako chini ya shirki, basi anaingia ndani ya matakwa ya Allaah:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[3]

[1] 04:48

[2] 4:31

[3] 4:48

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 16/08/2021