77. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi na tano wa Aal ´Imraan

al-´Ayyaashiy amesema:

“Yuunus bin Dhwibyaan amesema: “Nilimuuliza Abu Ja´far kuhusiana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ

“Na madhalimu hawana yeyote mwenye kuwanusuru.”[1]

Akajibu: “Hawana maimamu waliowapa majina yao.”[2]

Wanawalenga Maswahabah na wafuasi wao waislamu ambao wanashikamana na dini ya haki na hawaamini uongo wa Raafidhwah. Upande mmoja Aayah inahusiana na makafiri na ina maana ya kwamba hakuna yeyote atakayewalinda dhidi ya adhabu ya Allaah. Upande mwingine Raafidhwah wanawapachika nayo Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 03:192

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/211).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 115
  • Imechapishwa: 13/04/2017