Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Yaweza kusemwa pia: “Wale ambao ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) aliwaunguza kwa moto, wote walikuwa wakidai Uislamu. Walikuwa ni katika wafuasi wa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) na walisoma elimu kutoka kwa Maswahabah, lakini waliitakidi kwa ´Aliy kama inavyoitakidiwa kwa Yuusuf, Shamsaan na mfano wao. Vipi waliafikiana Maswahabah kuwapiga vita na kuwaona kuwa ni makafiri? Je, mnadhani ya kwamba Maswahabah wanawakufurisha waislamu au mnadhani ya kwamba kuwa na imani kwa Taaj na mfano wake haidhuru, wakati kuwa na imani kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib ndio kunakufurisha?

Yaweza kusemwa pia: “Banuu ´Ubayd al-Qaddaah, waliokuwa wakimiliki Magharibi [ya Afrika] na Misri katika zama za Banuu al-´Abbaas, wote walikuwa wakishuhudia ya kuwa hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Walikuwa wanadai Uislamu, wanaswali ijumaa na swalah za mikusanyiko. Ilipodhihiri kukhalifu kwao Shari´ah katika mambo fulani ambayo sisi hatuyafuati, walikubaliana wanachuoni kuwa ni makafiri na kwamba inatakiwa kuwapiga vita na kwamba miji yao ni miji ya vita. Hivyo waislamu wakawashambulia mpaka wakaokoa waliokuwa nayo katika miji ya waislamu.”

MAELEZO

Hili ni jibu la tano. Wanazuoni walikubaliana kuwa Banuu ´Ubayd al-Qaddaah ni makafiri. Walikuwa wakimiliki Magharibi na Misri na wakishuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Walikuwa wanaswali ijumaa na swalah za mikusanyiko na wakidai Uislamu. Pamoja na hivyo hili halikuwazuia waislamu kuwahukumu kuritadi pale ilipodhihiri kwenda kinyume na waislamu katika baadhi ya mambo. Hatimaye wakawapiga vita na wakavichukua vile walivyokuwa wakivimiliki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 86-87
  • Imechapishwa: 25/11/2023