Madhambi makubwa ni yale yamepangiwa adhabu duniani, kama mfano wa uzinzi, wizi na unywaji pombe, au matishio ya adhabu huko Aakhirah, kama mfano wa kupatwa na ghadhabu za Allaah na Moto. Kila dhambi iliyotajwa ikaambatanishwa na adhabu huko Aakhirah basi ni dhambi kubwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا

“Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhuluma, hapana shaka kwamba wanakula ndani ya matumbo yao moto na watauingia moto uliowashwa vikali mno.”[1]

Kwa msemo mwingine ni kwamba madhambi makubwa ni yale yaliyopangiwa kutekelezewa adhabu duniani, matishio huko Aakhirah, laana au ghadhabu za Allaah. Madhambi mengine yote ni madogo yanayofutwa kwa yale tuliyoyataja. Allaah (Ta´ala) amesema:

الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ

“… wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu isipokuwa makosa madogomadogo. Hakika Mola wako ni mkunjufu wa msamaha.”[2]

[1] 4:10

[2] 53:32

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 58
  • Imechapishwa: 16/08/2021