75. Hali tatu mtu anaposahau Tashahhud ya kwanza

Zipo hali tatu pale ambapo mtu anasahau Tashahhud ya kwanza:

1 – Akakumbuka kabla hajasimama kunyooka sawasawa. Katika hali hii analazimika kurejea na asujudu sijdah ya kusahau.

2 – Akakumbuka baada ya kwamba ameshasimama kunyooka sawasawa lakini kabla ya kuanza kusoma. Bora kwa mtu huyu ni kuendelea na asirejee. Akirejea imechukizwa juu yake.

3 – Asikumbuke isipokuwa baada ya kuanza kusoma al-Faatihah. Katika hali hii imeharamishwa kwake kurejea. Kwa sababu atakuwa ameichanganya na nguzo nyingine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 108
  • Imechapishwa: 04/07/2022