76. ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya mizani


Mwandishi (Rahimahu Allaah) amesema

wala [usipinge] hodhi na mizani – hakika wewe unanasihiwa

La tatu: Mizani. Ni mizani ya kihakika ilio na masahani mawili. Mema yatawekwa kwenye sahani moja na maovu kwenye sahani lingine. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ

“Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito – hao ndio wenye kufaulu, na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu – basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao [watakuwa] kwenye [Moto wa] Jahannam ni wenye kudumu.” (23:102-103)

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ  فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ  وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ  فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ

“Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito, basi huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha, na yule itakayekuwa mizani yake khafifu, basi makazi yake [itakuwa] ni Haawiyah.” (101:06-09)

Mizani hapa bi maana matendo yake. Mame yake yatawekwa kwenye sahani moja na maovu yake yatawekwa kwenye sahani lingine. Atalipwa kutegemea na ule upande utaokuwa na uzito zaidi. Haya ni kutokana na uadilifu wa Allaah. Hamdhulumu yeyote. Bali anamlipa mwanaadamu kwa matendo yake. Ni mizani ya kihakika.