75. Wataokunywa na kuzuiwa na Hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

Ambaye alishikamana na Sunnah za Mtume duniani na akazitendea kazi ndiye ambaye ataifikia Hodhi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Qiyaamah na atakunywa kutoka humo. Kuhusu ambaye aliipuuza Sunnah na akazua Bid´ah au akaritadi kutoka katika dini yake, atatimuliwa na kufukuzwa kutoka kwenye hiyo Hodhi ilihali kipindi hicho ndio atakuwa na haja kubwa kabisa ya maji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 166
  • Imechapishwa: 13/01/2024