75. Wataokunywa na kuzuiwa na hodhi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)


Ambaye alishikamana na Sunnah za Mtume duniani na akazitendea kazi ndiye ambaye ataifikia hodhi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Qiyaamah na atakunywa kutoka humo. Kuhusu ambaye aliipuuza Sunnah na akazua Bid´ah au akaritadi kutoka katika dini yake, atatimuliwa na kufukuzwa kutoka kwenye hiyo hodhi ilihali kipindi hicho ndio atakuwa na haja kubwa kabisa ya maji.