75. Kutumiwe mawe kusipopatikana matofali ya udongo?


Swali 75: Kutumiwe mawe kusipopatikana matofali ya udongo?

Jibu: Kusipopatikana matofali ya udongo italazimika kutumia mawe, vibao, miti au vyenginevyo miongoni mwa vile vitu vinavyomlinda maiti. Kisha atafunikwa udongo juu yake kutokana na Aayah iliotangulia. Nayo ni maneno Yake (Subhaanah):

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… na yale niliyokuamrisheni basi yaendeeni kiasi muwezavyo.”[2]

[1] 64:16

[2] Ahmad (7288) na Muslim (1337).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 55
  • Imechapishwa: 31/12/2021