74. Kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah V


Mwenye kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah kutokana na kukosea katika Ijtihaad yake, midhali ni mwenye kustahiki kufanya hivo, na akawa hakukusudia kwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Amekusudia kuhukumu kwa mujibu wa yale aliyoteremsha Allaah, lakini hata hivyo hakuwafikishwa usawa. Huyu ni kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Akijitahidi hakimu na akapatia, basi ana ujira mara mbili, na akijitahidi na akakosea, basi ana ujira mara moja.”[1]

Kosa lake linasamehewa. Hakukusudia jambo hili. Ni mwenye kupupia kuhukumu kwa mujibu wa Shari´ah ambapo akajitahidi na anapekua hukumu ya Kishari´ah. Lakini hata hivyo hakuwafikishwa. Huyu anapewa thawabu kwa Ijtihaad na nia yake na kosa lake linasamehewa kwa sababu hakukusudia kosa hili.

Huu ndio ufafanuzi katika masuala haya makubwa ambayo ndio tatizo kubwa la leo.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy (7352) na Muslim (1716).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 103
  • Imechapishwa: 13/11/2018