Aliyepatwa na msiba anatakiwa kutambua kuwa aliyempa majaribio ya msiba ni yule mwadilifu kabisa wa kuhukumu na mwenye huruma kabisa wa walio na huruma. Anatakiwa kutambua ya kwamba (Subhaana) hakumpa majaribio ili kumpa pigo, kumuadhibu wala kumuharibu. Amefanya hivo ili kumjaribu subira yake, alivyo radhi na Yeye na anavyomuamini. Amefanya hivo ili aone unyenyekevu wake Kwake na kumuona ni mwenye kunyenyekea kwenye mlango Wake akimuomba msaada Wake. Katika hali hii ananyanyua mikono yake mbele Yake na kumshtakia Yeye. Shaykh na Imaam ´Abdul-Qaadir al-Kaylaaniy (Rahimahu Allaah) alisema kumwambia mtoto wake:

“Ee mwanangu! Msiba haukuja kwa ajili ya kutaka kukuangamiza. Umekuja ili kuijaribu subira na imani yako. Ee mwanangu! Makadirio ni mnyamamkali na mnyamamkali hali nyamafu.”

Makusudio ni kwamba msiba ni moto wa mja anaousafishia bidhaa; ima dhahabu itoke au kila kitu kiungue.

Mja asiponufaika na moto wa hapa duniani basi unamsubiri Moto mkubwa wa huko Aakhirah. Mja akijua kuwa ni bora kwake kuuingia moto wa hapa duniani kuliko Moto wa huko Aakhirah na kwamba ni lazima akutane na mmoja katika hiyo miwili, basi atatambua ukubwa wa neema ya Allaah aliyomtunuku kwa kumfanya aingie moto wa hapa duniani. Pindi Allaah anapopanga mja kupatwa na msiba hapa duniani, basi anatakiwa kusubiri katika kile kipindi cha kwanza msiba unamgonga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 166
  • Imechapishwa: 12/11/2016