74. Ikiwa ardhi ni ya milima azikwe maiti katika mapango au mageto?


Swali 74: Ikiwa ardhi ni ya milima azikwe maiti katika mapango au mageto[1]?

Jibu: Kama kuna wepesi wa kumchimbia kaburi na likazungushiwa mawe, basi ndio bora kuliko mapango. Isiposahilika kufanya hivo basi atawekwe ndani ya pango na kuhifadhiwa mpaka asalimike kutokamana na wanyama wakali na wengineo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/190).

[2] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 31/12/2021