Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ummah huu umefaradhishiwa kufanya Hijrah kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu na itabaki mpaka Qiyaamah kitaposimama. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚقَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, wataambiwa: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.”  Malaika watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa pana mkahajiri ndani yake?” Basi hao makazi yao yatakuwa ni Moto – na ubaya ulioje mahali pa kurejea! Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata namna yoyote wala hawawezi kuongoza njia. Basi hao huenda Allaah akawasamehe – na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufiria.” (an-Nisaa´ 04 : 97-99)

MAELEZO

Ummah huu umefaradhishiwa kufanya Hijra… – Hijrah ni wajibu kwa kila muumini asiyeweza kudhihirisha dini yake katika nchi ya kikafiri. Ikiwa hawezi kudhihirisha Uislamu, basi Uislamu wake unakuwa mpungufu mpaka afanye Hijrah. Jambo lolote lisilotimia isipokuwa kwa kufanya jambo hilo, basi jambo hilo litakuwa ni wajibu pia.

Hakika wale ambao Malaika wamewafisha… – Katika Aayah hii kuna dalili kuwa wale ambao hawakuhajiri ilihali wana uwezo wa kufanya Hijrah, Malaika watawafisha. Kisha watawasema vibaya na kuwaambia:

أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا

“Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa pana mkahajiri ndani yake?”

Ama wale wasioweza na wanyonge, Allaah amewasamehe kwa kutoweza kwao kufanya Hijrah. Allaah haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa uwezo wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 130
  • Imechapishwa: 03/06/2020