73. Maiti anawekwa vipi ndani ya kaburi lake?


Swali 73: Maiti anawekwa vipi ndani ya kaburi lake[1]?

Jibu: Hadiyth ya ´Abdullaah bin Zayd imefahamisha kuwa maiti anaingizwa upande wa miguu yake na atateremshwa kulazwa upande wake wa kulia na huku uso wake umeelekezwa upande wa Qiblah. Hivi ndivo bora na Sunnah. Sunnah wakati wa kumweka katika mwanandani aseme yule mwekaji:

بسم الله وعلى ملة رسول الله

“Kwa jina la Allaah na juu ya mila ya Mtume wa Allaah.”

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/189-190).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 54
  • Imechapishwa: 31/12/2021