73. Kuwarudisha viumbe kuna wepesi zaidi


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah atawafufua waliokufa. Kama alivyowaumba mwanzoni basi atawarudisha.

MAELEZO

Kama alivyowaumba mara ya mwanzo basi atawarudisha kuwa hai kwa idhini Yake kwa mara nyingine kama mlivyokuwa mara ya kwanza. Yule ambaye ameweza kuwaanzilisha basi ana haki zaidi ya kuweza kuwarudisheni. Amesema (Ta´ala):

وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ ۚ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

”Naye ndiye aliyeanzisha uumbaji, kisha anaurudisha, nayo ni mepesi mno Kwake. Naye ana wasifu wa juu kabisa katika mbingu na ardhi. Naye ni Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye hekima ya kila jambo.”[1]

[1] 30:27

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 57
  • Imechapishwa: 12/08/2021