73. Kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah IV

Kuhusu mwenye kuitakidi ya kwamba haijuzu kuhukumu kinyume na aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akaitakidi ya kwamba haijuzu kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah (´Azza wa Jall), lakini hata hivyo akaenda kinyume nayo kwa sababu ya matamanio ndani ya nafsi yake pamoja na kuamini kuwa kafanya maasi na tendo la haramu, lakini shahawa na matamanio yamemfanya akahukumu kinyume na hukumu ya Allaah au kilichomfanya akafanya hivo ni tamaa ya kidunia kama ruhswa na pesa na matokeo yake akahukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah. Yote hii ni tamaa ya pesa. Sambamba na hilo anaamini kuwa ni mtenda maasi na kaenda kinyume na amri ya Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inawezekana vilevile kwamba amehukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah kwa sababu ya kutaka kupata nafasi na wakati huohuo anaona kuwa amekosea na kwamba kitendo chake hichi hakijuzu. Mtu kama huyu hakufuru kufuru inayomtoa katika Uislamu isipokuwa anakufuru kufuru ndogo isiyomtoa katika Uislamu. Inahusiana na kufuru ndogo, kama alivyosema Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa)[1]. Huyu ndiye ambaye anakufuru kufuru aina ndogo. Mwenye kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah kwa sababu ya matamanio yaliyomo moyoni mwake, si kwa sababu anaona kuwa kufanya hivo inafaa, ni bora au ni sawa, lakini matamanio ndio yamempelekea akafanya hivo, tamaa ya pesa na cheo na matokeo yake akahukumu kinyume na hukumu ya Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu ya jambo hili lililompelekea pasi na kuwa na imani fulani. Hii ndio huitwa kufuru ya kimatendo. Nayo ni kufuru ndogo. Lakini ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa na ya khatari sana. Lakini mwenye nayo hahukumiwi kuwa katoka katika Uislamu. Kwa kuwa imani yake bado ni yenye kubaki.

[1] Ibn Jariyr (06/306-308), Ibn Haatim (04/1143) na al-Haakim (02/313).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 13/11/2018