73. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi wa Aal ´Imraan


al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ

“Kila nafsi itaonja mauti. Hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na Moto na akaingizwa basi amefuzu. – na haukuwa uhai wa dunia chochote isipokuwa ni starehe ya udanganyifu.[1]

“Mama yangu amenieleza, kutoka kwa Sulaymaan ad-Daylamiy, kutoka kwa Abu Baswiyr, kutoka kwa Abu ´Abdillaah aliyesema: “Itapofika siku ya Qiyaamah Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ataitwa ambapo atapewa nguo halafu akae upande wa kulia wa ´Arshi. Halafu aitwe Ibraahiym (´alayhis-Salaam) apewe nguo nyeupe na halafu akae upande wa kushoto wa ´Arshi. Kisha aitwe kiongozi wa waumini ´Aliy ambapo atapewa nguo na kukaa upande wa kulia wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Halafu aitwe Ismaa´iyl (´alayhis-Salaam) ambapo atapewa nguo nyeupe na kukaa upande wa kushoto wa Ibraahiym. Halafu ataitwa al-Hasan ambapo atapewa nguo na kukaa upande wa kulia wa kiongozi wa waumini. Kisha aitwe al-Husayn ambapo atapewa nguo na kukaa upande wa kulia wa al-Hasan. Halafu wataitwa maimamu ambapo kila mmoja atapewa nguo na kusimama upande wa kulia wa mwenzie. Kisha wataitwa Shiy´ah ambapo watasimama mbele yao. Kisha ataitwa Faatwimah na wanawake wake kutoka katika kizazi chake na wafuasi wake waingie Peponi pasi na hesabu. Kisha aitwe mwenye kuita kwenye ´Arshi na kutoka upande wa mwenye nguvu na kwa Mola juu: “Ni uzuri uliyoje wa baba ulonae, ee Muhammad, ambaye ni Ibraahiym. Ni uzuri uliyoje wa ndugu ulionae, ambaye ni ´Aliy bin Abiy Twaalib. Ni wajukuu wazuri walioje ulionao ambao ni al-Hasan na al-Husayn. Ni kipomoko kizuri kilichoje ulichonacho ambacho ni Muhsin. Ni maimamu waongofu gani ulionao kutoka katika kizazi chako. Ni wafuasi wazuri walioje ulionao katika wafuasi wako. Hakika Muhammad, wasii wake, wajukuu wake na maimamu kutoka katika kizazi chake ndio wenye kufuzu.” Kisha awaingize Peponi.”[2]

Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah kutokamana na uongo huu mkubwa. Tazama uongo na uzushi huu! ´Aliy, maimamu na Raafidhwah wako upande wa kulia wa ´Arshi ilihali Ibraahiym na Ismaa´iyl wako upande wake wa kushoto.

Kiko wapi kizazi cha Ibraahiym na Ishaaq, Ya´quub, Yuusuf, Muusa, Daawuud, Sulaymaan, ´Iysaa na Mitume wengine wa wana wa Israaiyl? Wako wapi Manabii na Mitume wengine wote (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam)? Yuko wapi Muhammad na Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam)? Wako wapi wasichana wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Wako wapi Banuu Haashim wengine waliobaki? Iko wapi dhuriya nyingine ya ´Aliy iliobaki?

Wafuasi wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanawake wao wataingia Peponi wakati Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakeze wataingia Motoni. Au kwa msemo wa sawa wafuasi wa Ibn Sabaa´ – yaani Raafidhwah Baatwiniyyah – wataingia Peponi wakati Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wataingia Motoni. Laana ya Allaah iwe juu ya waongo ambao wanazuilia njia ya Allaah na wanataka kuipotosha na wanamzulia Allaah uongo!

[1] 03:185

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/128).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 112-113
  • Imechapishwa: 13/04/2017