Swali 72: Ni ipi bora kufanya mwanandani ulio karibu na ukuta upande wa Qiblah[1] na mwanandani katikati ya kaburi[2]? Kaburi linanyanyuliwa kwa kiasi gani[3]?

Jibu: Madiynah walikuwa wakifanya mwanandani upande wa Qiblah na wakati mwingine wanachimba mwanandani katikati ya kaburi. Mwanandani upande wa Qiblah ndio bora zaidi. Kwa sababu Allaah amemchagulia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kutengeneza mwanandani katikati ya kaburi inafaa na khaswa pale ambapo kunahitajika kufanya hivo. Hadiyth ya Ibn ´Abbaas isemayo:

“Mwanandani upande wa Qiblah ni kwa ajili yetu na mwanandani katikati ya kaburi ni kwa ajili ya wengine.”

ni dhaifu. Katika cheni ya wapokezi wake yuko mtu anayeitwa Abul-A´laa ath-Tha´labiy ambaye ni mnyonge.

Kaburi linanyanyuliwa kiasi cha shibiri na karibu au kukaribia hivo.

[1] Lahd.

[2] Shaqq.

[3] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/189).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 53-54
  • Imechapishwa: 31/12/2021