72. Kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah III


Vivyo hivyo yule mwenye kusema kwamba hukumu ya Allaah ni haki lakini hata hivyo si lazima kwa watu kuitumia. Akaona kuwa inajuzu kwa watu kuhukumu kwa hukumu nyingine na kwenda na wakati pindi atapoona manufaa ya kufanya hivo. Mtu kama huyu ni mwenye karitadi kutoka katika dini ya Uislamu. Kwa sababu haijuzu kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah (´Azza wa Jall). Kila hukumu kinyume na hukumu ya Allaah basi ni batili. Jengine ni kwamba haitatui matatizo. Bali inazidisha matatizo zaidi. Ukimwambia mtu kwamba hii ni hukumu ya Allaah (´Azza wa Jall), basi hana jengine isipokuwa kuikubali hukumu ya Allaah:

إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا

“Hakika kauli ya waumini wa kweli wanapoitwa kwa Allaah na Mtume wake ili awahakumu kati yao, basi husema: “Tumesikia na Tumetii.” (an-Nuur 24:51)

Bi maana hapana khiyari ya mtu katika hukumu ya Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia ya kwamba akitaka ataikubali na asipotaka ataikataa. Lakini unachoweza kufanya ni kusamehe haki yako. Hili ni jambo jengine. Ama kusema kwamba hukubali na kwamba unaenda katika mahakama ya kikanuni. Huku ni kuritadi kutoka katika dini ya Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 101-102
  • Imechapishwa: 12/11/2018