Mtazamo wa pili wa kilimwengu: Mtazamo sahihi.

Mtu anayachukulia yaliyomo katika maisha haya katika mali, ufalme, nguvu za kiuchumi kuwa ni njia zinazomsaidia kwa ajili ya kuitendea kazi Aakhirah.

Ukweli ni kwamba ladha za dunia hazisemwi vibaya. Kusifiwa na kusemwa vibaya itategemea na yale anayofanya mja ndani yake. Ni kivukio cha kwenda Aakhirah na ni akiba ya Peponi. Maisha mazuri waliyopata watu wa Peponi ni kwa sababu ya yale waliyopanda duniani. Kwa hiyo ni nyumba ya mapambano, kuswali, kufunga, kujitolea katika njia ya Allaah na mashindano kwenda Aakhirah. Allaah (Ta´ala) anasema kuhusu watu wa Peponi:

كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ

“Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilopita.”[1]

[1] 69:24

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 136
  • Imechapishwa: 06/04/2020