70. Watu watakaokumbana na Qiyaamah

Mahdiy ni moja katika alama kubwa. Anatokamana na kizazi cha al-Hasan bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye atajitokeza katika kipindi ambacho kumejaa tofauti. Watu watakula kwake kiapo cha usikivu na utiifu na serikali yake itakuwa nzuri. Ulimwengu utajaa uadilifu kama ulivyokuwa umejaa dhuluma na atapambana katika njia ya Allaah. Mwishoni mwa zama za al-Masiyh ad-Dajjaal atajitokeza al-Masiyh ad-Dajjaal. Inahusiana na fitina kubwa na msiba mkuu. Kisha atashuka al-Masiyh, mwana wa Maryam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), atamuua ad-Dajjaal. Hatimaye waislamu wasalimike kutokamana na shari yake. Baadaye ajitokeza Ya´juuj na Ma´juuj. Hizi ni lama za Qiyaamah kubwakubwa ambazo zitafululiza. Allaah atazichukua roho za waumini kabla ya hapo na hakuna watakaobaki isipokuwa waovu peke yao. Hatokuweko yeyote mwenye kumtaja Allaah. Qiyaamah kitakumbana na wale wataokuwa wanaishi kipindi hicho. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika miongoni mwa waovu kabisa wa watu ni wale ambao Qiyaamah kitawakuta wakiwa hai na wale wanaoijenga misikiti juu ya makaburi.”[1]

Alama nyingine ni moto utakaowafukuza watu kuelekea uwanja wa Mkusanyiko. Utakesha usiku pale wanapokesha na utalala na wao mchana pale wanapolala mchana. Kwa mujibu wa Hadiyth Moto huo utatokea Aden[2]. Hizi ni lama zilizoelezwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadhi yake zimetajwa ndani ya Qur-aan. Lakini ni lini khaswa Qiyaamah kitatokea? Hakuna anayejua hilo isipokuwa Allaah.

[1] Ahmad (3844), Ibn Khuzaymah (789), Ibn Hibbaan (6847) na at-Twabaraaniy (10413). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”ath-Thamar al-Mustatwaab” (1/363).

[2] at-Tirmidhiy (2183).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 11/08/2021