Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

“Nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”

Nakiri, natambua, nasadikisha na nashuhudia hali ya kuwa na yakini ya kwamba Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Abdil-Muttwalib bin ´Abdil-Manaaf al-Haashimiy al-Qurashiy mwarabu wa Makkah kisha akaenda Madiynah kwamba ni Mtume wa Allaah.

Maneno yake:

“Kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah ina maana ni mja asiyeabudiwa na ni Mtume asiyekadhibishwa.”

unashuhudia ya kuwa ni mja asiyeabudiwa na ni Mtume asiyekadhibishwa. Yeye ni mja wa Allaah (Ta´ala). Yeye ndiye mtu mkubwa zaidi anayemwabudu Allaah (´Azza wa Jall). Yeye ndiye mkubwa zaidi wa watu inapokuja katika jambo la kutakasa ´ibaadah. Yeye ni Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mtunzi amesema:

“… bali anatiiwa na kufuatwa… “

Ni lazima kwa muislamu kusadikisha maelezo yake, kumtii, kumfuata, kunyenyekea hukumu zake na amwabudu Allaah (Ta´ala) kwa yale aliyoyaweka katika Shari´ah. Aidha ayatangulize mbele mapenzi yake juu ya kupenda pesa, nafsi, mtoto na kila kitu.

Mtunzi amesema:

Allaah Kamtukuza kwa kuwa mja. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَى عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا

“Amebarikika Yule ambaye ameteremsha Pambanuzi kwa mja Wake ili awe ni muonyaji kwa walimwengu.”

Kinacholengwa ni maneno Yake:

عَلَى عَبْدِهِ

”… kwa mja Wake… ”

Amemsifu kwa uja katika maeneo ya kuteremsha Qur-aan. Vivyo hivyo katika maeneo ya kumsafirisha usiku pale aliposema (Ta´ala):

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا

“Utakasifu ni wa Ambaye amemsafirisha mja Wake usiku.”[1]

Vilevile katika maeneo ya ulinganizi pale aliposema (Ta´ala):

وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ

“Pindi mja wa Allaah aliposimama kumwomba.”[2]

Pia katika maeneo ya kutoa changamoto pale aliposema (Ta´ala):

وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا

”Ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya mja Wetu.”[3]

[1] 17:01

[2] 72:19

[3] 02:23

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 100
  • Imechapishwa: 29/06/2022