Mwenye kudai ya kwamba wakati umebadilika na kwamba kuhukumu kwa Qur-aan na Sunnah ni mambo ya zamani yamepitwa na wakati na kwamba hali ya sasa inapelekea kuletwa hukumu ambazo zinaenda sambamba na wakati huu, kama wanavosema, huku ni kuritadi kutoka katika dini ya Kiislamu. Mwenye kuona kwamba kuhukumu kwa Shari´ah ni jambo haliendani na wakati wa leo na kwamba inatakikana kuleta hukumu na sheria za wanaadamu zinazoendana na wakati wa sas – kwa madai yao – huku ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall). Kwa sababu Shari´ah ni yenye kuendana na kila zama na mahali mpaka Qiyaamah kisimame. Ni wajibu kuitakidi hivi. Ikiwa hakubainikiwa na uzuri wake, haya ni katika upungufu wake yeye na upungufu wa uelewa wake na si kwamba Shari´ah ni pungufu.

Kuna ambao wanasema kwamba kusimamisha adhabu za Kishari´ah kama vile kumpiga mawe mzinifu, kuukata mkono mwizi na kumuua mwenye kuritadi ya kwamba eti hizi ni hukumu ambazo haziendani na zama za leo za maendeleo kwa sababu watu fikira na akili zao zimeendelea. Wanaona kuwa kusimamisha hukumu za Shari´ah ni jambo haliendani na wakati wa leo na kwamba mwenye kuua asisimamishiwe adhabu. Wanasema kuwa haya ni matendo ya unyama. Haya ni maneno ambayo yanatoka kwa baadhi ya wanafiki. Huku ni kuritadi kwa wazi na ni kutoka katika dini ya Uislamu. Kwa sababu ni kupingana na hukumu ya Allaah na kuitakidi kuwa hukumu ya Allaah ni yenye mapungufu na haifai. Huku ni kuritadi kwa wazi kutoka katika dini ya Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 12/11/2018