70. Je, imesuniwa kusimama juu ya jeneza la kafiri?

Swali 70: Je, imewekwa katika Shari´ah kusimama juu ya jeneza la kafiri[1]?

Jibu: Ndio, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kusimama juu ya kila jeneza kutokana na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtakapoona jeneza basi simameni.”[2]

Imepokelewa katika baadhi ya mapokezi?

“Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Hakika ni jeneza ya myahudi.” Akasema: “Kwani sio nafsi?”[3]

Imekuja katika tamko lingine:

“Hakika si venginevyo tumesimama kwa ajili ya Malaika.”[4]

 Imekuja katika tamko lingine:

“Hakika kifo kinatisha.”[5]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/188).

[2] Ahmad (10811), al-Bukhaariy (1310-1311) na Muslim (958).

[3] Ahmad (23330), al-Bukhaariy (1313) na Muslim (961).

[4] Ahmad (18997, 19206).

[5] Ahmad (14398), an-Nasaa´iy (1922) na Abu Daawuud (3147).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 52
  • Imechapishwa: 30/12/2021