70. Du´aa baada ya kumaliza kula

  Download

180-

الْحَمْـدُ للهِ الَّذي أَطْعَمَنـي هـذا وَرَزَقَنـيهِ مِنْ غَـيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلا قُوَّةٍ

”Himdi zote ni stahiki ya Allaah ambaye amenilisha mimi [chakula] hichi na akaniruzuku pasi na uwezo wala nguvu zangu.”[1]

181-

الْحَمْـدُ للهِ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُبـارَكاً فيه، [غَيْرَ مَكْفِيٍّ] وَلا مُوَدَّعٍ وَلا مُسْتَغْـنىً عَنْـهُ رَبُّـنا

“Himdi anastahiki Allaah, himdi nyingi, nzuri, zenye baraka ndani yake [zisizotoshelezwa] wala kuagwa, wala kutoshwa nazo, Mola wetu.”[2]

[1] Watunzi wa “as-Sunan” isipokuwa an-Nasaa´iy. Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/159).

[2] al-Bukhaariy (06/214) na at-Tirmidhiy (5/507) kwa tamko lake.

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 02/05/2020