7 – Ulinganizi wa Uislamu wa kwa jumla ndio ilikuwa Da´wah ya Hasan al-Bannaa

Baadhi ya ndugu waaminifu wamenieleza mkutano wa Hasan al-Bannaa (Rahimahu Allaah) (ambapo alikuwa pamoja na baadhi ya viongozi wa al-Ikhwaan al-Muslimuun) na raisi mkuu wa Answaar-us-Sunnah al-Muhammadiyyah Shaykh Muhammad Haamid al-Faqiy (Rahimahu Allaah) kwenye chumba cha ´Aabidiyn. Shaykh alikuwa pamoja na baadhi ya ndugu. Hasan al-Bannaa akaja na fikra ya kushirikiana katika Da´wah. Ndipo Shaykh Muhammad Haamid al-Faqiy akauliza:

“Tutalingania katika nini?” Hasan al-Bannaa akasema: “Katika Uislamu kwa jumla.” Shaykh Muhammad al-Faqiy akasema: “Basi tuanze kulingania katika Tawhiyd, ´Aqiydah ya Ahl-uS-Sunnah wal-Jamaa´ah.” Hasan al-Bannaa akapinga kwa kusema: “Hivo watu watatuacha.”

Kila mmoja abaki katika msimamo wake. Baada ya hapo wakakutana mara nyingi na hawakupatana. Kila mmoja aendelee na usulubu wake alioanza nao.

Miongoni mwa ambao walinieleza mkutano huu ni kaka yangu Shaykh Muhammad [bin ´Abdil-Wahhaab al-Bannaa] na Ahmad Ghariyb.

Shaykh ´Abdul-´Aziyz Aashuur ameeleza kuwa baba yake alisema:

“Shaykh Muhammad Haamid al-Faqiy alikutana na Hasan al-Bannaa na vigogo wa Mu´attwilah. Shaykh akamwambia Hasan al-Bannaa:

“Wewe hamu yako ni kukusanya tu kadiri na inavyowezekana.”

Na akawaambia Mu´attwilah:

“Msisemi kuwa mnamuabudu Allaah. Mungu wenu hana sifa wakati Allaah ana majina na sifa zilizothibitishwa katika Qur-aan na Sunnah.”

  • Mhusika: Shaykh Hasan bin ´Abdil-Wahhaab al-Bannaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Gazeti al-Asaas, uk. 53, ya ´Aliy al-Waswifiy Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 28-29
  • mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy