7. Nini maana ya imani kamilifu na inapanda na kushuka?


Swali 7: Ni nini maana ya imani kamilifu na inazidi na kupungua?

Jibu: Imani ni I´tiqaad za moyo na matendo, matendo ya viungo na maneno ya ulimi.

Dini yote, misingi yake na matawi yake vinaingia katika imani.

Ina maana ya kwamba inazidi kwa I´tiqaad yenye nguvu na wingi wake na matendo na maneno mazuri na mengi kama ambavyo inashuka kwa kinyume na hayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamm-ul-Muhimmaat, uk. 40
  • Imechapishwa: 25/03/2017