7. Kumtazama mtu unayetaka kuoana naye

Wakati mwanaume amepochukua maamuzi kihakika ya kumchumbia mwanamke, amwangalie. Ni katika haki za wanandoa katika mnasaba wa uchumbiaji. Imependekezwa ili amuoe kwa ujuzi na utambuzi. Ni sababu ya mapenzi yenye kuendelea na urafiki kati ya wanandoa ikiwa Allaah Ameamua kuwa wataoana. Pindi mwanamke anapojua kuwa mwanaume anataka kumuoa kwa sababu amemuona na amemchumbia kwa khiyari yake kwa sababu anamtaka, hushikwa na mapenzi na kumpenda zaidi. al-Mughiyrah bin Shu´bah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nilimwendea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza kuhusu mwanamke ambaye nimechumbia.” Akasema: “Nenda na umtazame. Kuna uwezekano
mkubwa uhusiano wenu ukabaki.”

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu akimchumbia mwanamke, ikiwa anaweza, basi
naangalie yale yenye kumvutia kuweza kumuoa.”
[1]

Kuna mtu alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza kuwa anataka kuoa mwanamke wa Answaar. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:

Je, umemwangalia?” Akajibu: “Hapana.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mwangalie. Hakika kuna kitu kwenye macho ya Answaar.”[2]

Ina maana ya kwamba kwenye macho ya wanawake wa ki-Answaar kulikuwa kuna kitu duni. Ili aweze kujua ni nani anayemwoa ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawa amemwambia:

“Mwangalie.”

[1] Abu Daawuud (2082) na Ahmad (3/334). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (1791) na ”as-Swahiyhah” (99).

[2] Muslim (1424)

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 24/03/2017