69. Ni lazima kusimama wakati linapopita jeneza?

Swali 69: Je, muislamu akiwa msikitini na akaona jeneza asimame[1]?

Jibu: Udhahiri wa Hadiyth ni ueneaji. Kwa hivyo imependekezwa. Ambaye ataacha kufanya hivo hapana shida. Kusimama ni jambo limependekezwa na sio lazima. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mara alisimama na mara nyingine aliacha. Kwa hiyo ikajulisha kwamba sio lazima.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/187-188).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 52
  • Imechapishwa: 30/12/2021