69. Maana ya sentesi ya shahaadah ya kwanza


Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

أشهد أن لا إله إلا الله و أشهد أن محمداً عبده و رسوله

“Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”

Unashuhudia shahaadah ya yakini ya kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki katika ardhi wala mbinguni isipokuwa Allaah. Kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah ina maana ni mja asiyeabudiwa na ni Mtume asiyekadhibishwa, bali anatiiwa na kufuatwa. Allaah Kamtukuza kwa kuwa mja. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَى عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا

“Amebarikika Yule ambaye ameteremsha Pambanuzi kwa mja Wake ili awe ni muonyaji kwa walimwengu.”[1]

MAELEZO

Maneno yake:

“Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah… “

Bi maana nakiri, natambua na kusadikisha.

Maneno yake:

“Unashuhudia shahaadah ya yakini… “

Hakuna mwabudiwa wa haki mbinguni na ardhini isipokuwa Allaah.

Wako waabudiwa wa batili kama mfano wa waabudia makaburi, waabudia Malaika, wako wanaoabudia miti, mawe na maji. Bali wako wenye kuabudia tupu. Inasemekana kwamba India wako waabudiwa wengi kukiwemo wanaoabudia tupu. Aidha wako waabudia shaytwaan. Wanamwabudu shaytwaan badala ya Allaah. Amesema (Ta´ala):

أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَا بَنِي آدَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ وَأَنِ اعْبُدُونِي ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ

“Je, Sijakukuahidini enyi wana wa Aadam kwamba: “Msimwabudu shaytwaan, hakika yeye kwenu ni adui bayana na kwamba Niabuduni Mimi Pekee – hii ndio njia iliyonyooka.””[2]

Hawa ni waabudiwa wa batili. Hakuna ´ibaadah ya haki isipokuwa kwa Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye wa haki na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili na kwamba Allaah ndiye Aliye juu kabisa, Mkubwa.”[3]

[1] 25:01

[2] 36:60-61

[3] 22:62

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 29/06/2022