69. al-Qummiy upotoshaji wake wa saba wa Aal ´Imraan

al-Qummiy amesema:

“Baba yangu amenieleza, kutoka kwa Ibn Abiy ´Umayr, kutoka kwa Ibn Sinaan aliyeseama: “Aayah:

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ

“Mmekuwa ni Ummah bora kabisa uliotolewa [katika na] kwa watu.”[1]

ilisomwa kwa Abu ´Abdillaah ambapo akasema: “Ummah bora wenye kumuua kiongozi wa waumini, al-Hasan na al-Husayn!?” Msomaji akasema: “Iliteremshwa vipi?” Akasema: “Namna hii:

كُنتُمْ خَيْرَ أئمّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ

“Mmekuwa ni maimamu bora kabisa uliotolewa [katika na] kwa watu.”

Huoni jinsi Allaah alivyowasifu:

تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ

“Mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamwamini Allaah.”[2]?[3]

1- Baatwiniy huyu anatilia nguvu na kuendelea kuipotosha Qur-aan.

2- Aayah hii inausifia Ummah huu, na khaswa khaswa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sifa ya pekee inayoupambanua na nyumati zingine zote. Baada ya Mitume hawana mfano katika historia ya uanaadamu. Hakujapatapo kuwepo na hakutokuwepo kamwe mfano wa Maswahabah. Kama kuna ambaye ni muumini anayeamrisha mema na kukataza maovu basi katika msitari wa mbele kabisa wanakuja Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Allaah amewatakasa katika Aayah nyingi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewatakasa kijumla na kibinafsi, jambo ambalo linapatikana katika Hadiyth Swahiyh. Amewashuhudilia Pepo waliokuwepo katika Hudaybiyah na wale kumi waliobashiriwa Pepo na khaswa khaswa Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). Kadhalika Allaah amesema kuhusu wale waliopigana vita vya Badr:

“Fanyeni mtakalo. Nimekusameheni.”

Hawa kumi ndio watu bora kabisa wa Ummah huu.

Katika mambo ambayo Maswahabah waliamrisha mema na kukataza maovu ni pamoja vilevile na kueneza Tawhiyd na kutokomeza shirki katika sehemu kubwa ya ardhi. Walitokomeza kuritadi katika kisiwa cha kiarabu na katika ardhi ya wafursi na warumi waliposhinda ambapo ulimwengu ukajaa nuru ya Uislamu na Tawhiyd na mpaka viza vya shirki na ukafiri vikapotea. Yote haya yalifanywa na wema hawa, watukufu na wapambanaji wakubwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Raafidhwah wao wamefanya nini? Wameufarikisha Ummah na kujitahidi kueneza shirki, dhuluma na upotevu. Hakuna yeyoye aliyeiudhi familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwakosesha nusura mpaka wakashindwa kuamrisha mema na kukataza maovu kama walivyofanya Raafidhwah. Hili ni jambo linalojulikana na kila ambaye yuko na uelewa mdogo kabisa. Haya yamejaa katika vitabu vya kihistoria.

[1] 03:110

[2] 03:110

[3] Tafsiyr al-Qummiy (1/110).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 105-106
  • Imechapishwa: 03/04/2017