68. Uwajibu wa kusoma al-Faatihah katika kila Rak´ah


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuamrisha yule mwanamume aliyeswali vibaya kusoma “al-Faatihah” katika kila Rak´ah. Baada ya kumuamrisha kuisoma katika ile Rak´ah ya kwanza akamwambia[1]:

“Halafu ufanye hivo katika swalah yako yote.”[2]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“… katika kila Rak´ah.”[3]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Katika kila Rak´ah kuna kisomo.”[4]

[1] Abu Daawuud na Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi ulio na nguvu.

[2] al-Bukhaariy na Muslim.

[3] Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi mzuri.

[4] Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na Ahmad katika ”Masaa-il-ul-Imaam Ahmad” (1/52) ya Ibn Haani’. Jaabir amesema:

”Atakayeswali Rak´ah pasi na kusoma “al-Faatihah” hakuswali isipokuwa akiwa nyuma ya imamu.” (Maalik)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 135-136
  • Imechapishwa: 20/08/2017