68. Kumwingiza maiti kupitia mlango ar-Rahmah katika msikiti wa Madiynah


Swali 68: Watu wengi al-Madiynah an-Munawarrah wamezowea kuwaingiza wafu wao kupitia mlango wa ar-Rahmah pasi na milango mingine. Wanaona kuwa kufanya hivo Allaah atamrehemu na kumsamehe. Je, kitu hichi kina usahihi wowote katika Shari´ah yetu iliyotakasika[1]?

Jibu: Sitambui imani hii kuwa na usahihi wowote katika Shari´ah pwekeshi. Bali hayo ni maovu na haijuzu kuonelea hivo. Hapana vibaya kuwaingiza wafu kupitia milango yote. Bora ni kumwingiza kupitia ule mlango ambao una madhara machache kwa waswaliji.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/187).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 51-52
  • Imechapishwa: 29/12/2021