Kujiunga na makundi ya kikafiri, kama ukomunisti, uanasekula, ubepari na mengineyo katika madhehebu ya kikafiri ni kuritadi kutoka nje ya Uislamu. Ikiwa yule aliyejiunga katika madhehebu hayo anadai Uislamu basi huo ni unafiki mkubwa. Kwani hakika wanafiki kwa uinjenje wanajiunga na Uislamu licha ya kuwa kwa undani ni makafiri. Amesema (Ta´ala):

وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ

“Wanapokutana na wale walioamini wanasema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao wanasema: “Hakika sisi tupamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwachezea shere tu.”[1]

الَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ اللَّـهِ قَالُوا أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَافِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوا أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ

”Wale wanaokungojeeni kwa uangalifu; inapokuwa ushindi ni kwenu kutoka kwa Allaa wanasema: ”Je, hatukuwa pamoja nanyi?” na inapokuwa kwa makafiri sehemu ya ushindi wanasema: ”Hatukuwa wenye kukudhibitini na tukakuzuilieni kutokamana na waumini?”[2]

Wanafiki hawa ni wenye hadaa. Kila mmoja wao ana sura mbili; sura aionyeshayo kwa waumini na sura aionyeshayo kwa nduguze makafiri. Vilevile wana ndimi mbili; ulimi mmoja anawabusu kwa uinje waislamu na ulimi mwingine akikutana na wenzake hubadilika:

وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ

“Wanapokutana na wale walioamini wanasema: “Tumeamini.” Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao wanasema: “Hakika sisi tupamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwachezea shere tu.”[3]

Wameipa mgongo Qur-aan na Sunnah kwa ajili ya kuwachezea shere na kuwadharau wenye navyo na wamekataa kunyenyekea hukumu ya Wahy mbili kwa kufurahikia ile elimu walionayo ambayo hainufaishi kitu kule kujikithirishia nayo isipokuwa shari na kiburi zaidi. Utawoana daima ni wenye kushikamana na Wahy hali ya kuuchezea shere:

اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ

“Allaah anawadhihaki wao na atawaendelez katika hali yao ya upetukaji mipaka wa kuasi wakitangatanga kwa upofu.”[4][5]

Allaah ameamrisha kujinga kwa waumini:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ

“Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli.”[6]

Madhehebu haya ya kikafiri ni yenye kuchukiana kwa sababu yamejengeka juu ya batili. Wakomunisti wanapinga uwepo wa Muumba (Subhaanahu wa Ta´ala) na wanazipiga vita dini za kimbingu. Ni nani anayeridhia akili yake kuishi bila imani na kupinga vyanzo vya kiakili na yenye yakini? Mtu kama huyu zimefunikwa akili zake. Wanasekula ni wenye kuzipinga dini na wanategemea uchumi usiyokuwa na mwelekeo. Hawana lengo katika maisha haya isipokuwa wanaishi kama wanyama. Wanabepari wao kazi ni kukusanya mali kwa njia yoyote ile na hawatazami halali wala haramu, hawana huruma wala upole kwa mafukara na masikini. Uchumi wao umejengeka juu ya ribaa ambayo ni kumpiga vita Allaah na Mtume Wake, ribaa ambayo imeziangamiza nchi na mtu mmojammoja na kunyonya damu ya wananchi ambao ni mafakiri. Ni mtu gani – sembuse yule ambaye ana chembe ya imani – anaridhia kuishi juu ya madhehebu haya bila ya akili, dini, malengo sahihi katika maisha yake anayoyalenga na isitoshe akajadiliana kwayo? Hakika si vyenginevyo madhehebu haya yamevamia nchi za Kiislamu pale ilipopotea katika nchi nyingi miongoni mwazo imepotea dini sahihi na zikaleleka juu ya upotevu na kuishi juu ya kufuata.

[1] 02:14

[2] 04:141

[3] 02:14

[4] 02:15

[5] Swifaat-ul-Munaafiqiyn, uk. 19 cha Ibn-ul-Qayyim.

[6] 09:119

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 31/03/2020