1 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule asiyewashukuru watu hamshukuru Allaah.”

2 – Yule aliyetendewa wema ni wajibu kwake kumshukuru kwa kufanya lililo bora zaidi au angalau basi afanye mfano wake. Kurudisha wema kama dalili ya shukurani hakuwezi kulinganishwa na kule kuanza ijapo itakuwa chache. Asiyeweza kupata kitu basi amsifu. Kwani wakati wa kutokuwa na uwezo kusifu kunachukua nafasi ya shukurani. Hakuna yeyote aliyejitosheleza na kushukuru.

3 – Muungwana hakufuru neema. Hakasiriki wakati wa msiba. Anashukuru wakati anapokuwa na neema. Anasubiri wakati anapokuwa na misiba. Asiyekuwa na shukurani kwa kidogo basi anakaribia kutoshukuru kwa kingi. Neema haziwi zenye kuongezeka isipokuwa pindi Allaah anaposhukuriwa na kisha yule aliyejitolea na vivyo hivyo majanga yanaondoshwa kwa njia hiyo.

4 – Ni wajibu kwa mwenye busara kushukuru neema anazopewa. Asifu wema aliofanyiwa kwa kiasi anavoweza. Akiweza basi afanye hivo maradufu, mfano wake au kwa kutambua neema hiyo inatokana na nani na kurudisha wema kwa shukurani. Aseme:

جزاك الله خيرا

“Allaah akujaze kheri.”

Asiyekuwa na kitu na hivyo akawa amesema hivo basi amemsifu hali ya juu.

5 – Miongoni mwa watu wako ambao wanazikufuru neema. Mmoja wao ni yule mtu asiyetambua sababu inayopelekea neema hizo au ni jinsi anatakiwa kuzishukuru kwa sababu hajui ni jinsi gani ya kutunza familia. Mtu kama huyo anatakiwa kupuuziliwa mbali. Mwingine ni yule mwenye kuelewa na akaacha kushukuru juu ya neema. Anamdharau yule aliyejitolea na neema yenyewe. Akiwa hivo basi ni lazima kwa mwenye busara asimpe tena na tena.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 263-267
  • Imechapishwa: 07/09/2021