Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”

Wamuombea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amani, rehema na baraka. Anaombewa, na wala haombwi pamoja na Allaah.

MAELEZO

Hii ni dalili juu ya kwamba hastahiki kuabudiwa. Wewe unamuombea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usalama, rehema na baraka. Kwa hiyo yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwenye kuhitaji. Mwenye kuhitaji hawi mungu wala mwabudiwa. Kuhusu Allaah hakuna yeyote amuombeaye usalama, rehema na baraka. Kwa sababu Yeye ndiye as-Salaam na amani inatoka Kwake. Yeye ndiye Mola wa wote na aliye juu yao. Hakuna yeyote aliye juu Yake mpaka aombewe. Hilo ni tofauti na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye ni kiumbe na ndiye mtu mtukufu zaidi. Allaah amemtukuza kwa unabii, ´ibaadah na ujumbe. Yeye ni mja na Mtume ambaye anatakiwa kutiiwa, kufuatwa, kusadikishwa na kupendwa zaidi ya inavopendwa pesa na nafsi. Lakini hata hivyo haabudiwi. ´Ibaadah ni haki ya Allaah. Yeyote anayemwabudu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi ameitekeleza haki ya Allaah kwenda kwa mwengine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 97
  • Imechapishwa: 28/06/2022