Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiinuka kwa kuegemea ardhi katika Rak´ah ya pili[1].

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikunja ngumi na akiitegemea mikono yake wakati anapoinuka[2].

Pindi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapofika juu katika Rak´ah inayofuata huanza kusoma “al-Faatihah” na wala hanyamazi[3].

Katika Rak´ah hii alikuwa anafanya kama anavyofanya katika ile Rak´ah ya kwanza isipokuwa tu alikuwa akiifanya kuwa fupi kidogo kuliko ile ya kwanza.

[1] ash-Shaafi´iy na al-Bukhaariy.

[2] Abu Ishaaq al-Harbiy kwa mlolongo wa wapokezi uliosalama. Maana kama hiyo imepokelewa na al-Bayhaqiy kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh. Kuhusiana na Hadiyth:

“Alikuwa akiinuka kama mshale bila ya kuegemea ardhini.”

 ni yenye kuzuliwa. Hadiyth zote zenye maana kama hiyo ni dhaifu. Yamebainishwa katika “adh-Dhwa´iyfah” (562, 929 na 968). Kuna mtu muheshimiwa alionelea kuwa kuupa kwangu nguvu mlolongo wa al-Harbiy ni tatizo ambapo nikalibainisha katika “Tamaam-ul-Minnah”. Rejea huko, ni muhimu.

[3] Muslim na Abu ´Awaanah. Hichi kipumziko kilichokanushwa inaweza kuwa kunamaanishwa kipumziko cha du´aa ya kufungulia swalah na sio kipumziko cha du´aa ya kuomba kinga dhidi ya shaytwaan. Inaweza pia kumaanisha zaidi ya hivyo, lakini naona kuwa chaguo la kwanza linakinaisha zaidi. Wanachuoni wana rai mbili juu ya du´aa ya kuomba kinga dhidi ya shaytwaan mbali na ile Rak´ah ya kwanza. Naonelea kuwa lililowekwa katika Shari´ah ni kuisoma katika kila Rak´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 135
  • Imechapishwa: 20/08/2017