67. Kuandika kalima ya Tawhiyd juu ya sanda au vitanda vya majeneza


Swali 67: Baadhi ya vitanda vya majeneza vinawekwa kalima ya Tawhiyd. Ni ipi hukumu yake[1]?

Jibu: Hili ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Kilichowekwa katika Shari´ah ni kumtamkisha shahaadah ambaye anataka kukata roho. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watamkisheni maiti wenu ´Laa ilaaha illa Allaah´.”

Ameipokea Muslim.

Makusudio ya maiti hapa ni wale wanaotaka kukata roho mpaka neno lao la mwisho liwe “Laa ilaaha illa Allaah”.

Kuhusu kuandika juu ya sanda au kaburi lake haijuzu.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/186).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 51
  • Imechapishwa: 29/12/2021