67. Baadhi ya mambo yanayofaa kati ya waislamu na makafiri II

Mambo ya kidunia, matangamano, kufanya biashara na makafiri, kubadilishana mambo ya kimanufaa kati ya waislamu na makafiri mambo ambayo hayaichafui dini, hakuna neno. Vielvile mambo ya kidiplomasia kati ya nchi na nchi, yote haya hayana neno. Washirikina walikuwa wakimtumia wajumbe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanazungumza na wanaingia kwake ilihali yuko ndani ya msikiti na kuongea. Mambo haya hayaingii katika kupenda. Bali ni katika manufaa yaliyoruhusiwa kati ya waislamu na makafiri. Ni wajibu kutofautisha kati ya haya mawili. Kwa sababu baadhi ya watu wanachanganya baina ya yanayojuzu na yasiyojuzu. Baadhi yao wanasema inajuzu kuwapenda na kuwafanya makafiri kuwa marafiki kwa sababu Allaah (Ta´ala) ameturuhusu kutaamiliana nao, kuoa wanawake wa Kitabu. Hivyo inajuzu kuwapenda na kutotofautisha baina yetu sisi na wao. Huyu ni mzembeaji. Upande mwingine wako wenye kuchupa mipaka na wasusuwavu ambao ambao wanaonelea kuwa haijuzu kuwa na uhusiano wowote na makafiri. Ni mamoja sawa iwe biashara, mambo ya safari, kuwalipiza wema na mengineyo. Wanaonelea kwamba kufanya hivi ni katika kuwapenda na kujenga nao urafiki. Tunamwambia kwamba kufanya mambo haya sio kuwapenda wala kujenga nao urafiki. Ni wajibu kutofautisha kati ya hayo mawili; kati ya uzembeaji na upetukaji mipaka. Dini ni kati na kati. Haina upetukaji wa mipaka wala uzembeaji.

Ni wajibu kwetu kuyajua mahusiano haya na makafiri, yanayojuzu na yasiyojuzu. Kwa kuwa hili ni jambo muhimu na khaswakhaswa katika zama hizi ambapo kumekithiri watu wanaozungumzia masuala ya dini pasi na elimu au wanazungumzia masuala ya dini kwa kufuata matamanio. Pengine wakawa na elimu lakini wanaongea kwa mujibu wa matamanio. Ni wajibu kwa mwanafunzi kujua hukumu ya Kishari´ah juu ya mambo haya. Hili ni jambo muhimu kwa kuwa linahusiana na ´Aqiydah ya muislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 95
  • Imechapishwa: 08/11/2018