66. Kumchelewesha maiti kutokana na manufaa fulani


Swali 66: Inafaa kuchelewesha mazishi ya mtu ambaye ana umuhimu katika Uislamu kwa mfano kwa muda wa siku tatu[1]?

Jibu: Ikiwa kuna maslahi katika kule kuchelewesha ni sawa. Ni kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alicheleweshwa ambapo alikufa siku ya jumatatu na hakuzikwa isipokuwa jumatano. Ikiwa kuna maslahi kama kufika kwa jamaa zake au mengineyo hapana shida.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/183).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 48
  • Imechapishwa: 28/12/2021