66. Kikao cha kupumzika


Halafu anakaa kwa kunyooka na akitilia uzito mguu wake wa kushoto mpaka kila mfupa unarudi mahala pake[1].

[1] al-Bukhaariy na Abu Daawuud. Kikao hichi kinajulikana kwa wanachuoni kama “kikao cha kupumzika”. Haya ndio maoni ya ash-Shaafi´iy na mfano wa hayo yamepokelewa kutoka kwa Ahmad, kama ilivyotajwa katika “at-Tahqiyq” (01/111). Maoni haya yanaendana na Ahmad kama inavyotambulika ni mwenye kusisitiza juu ya kufuata Sunnah isiyokuwa na kipingamizi. Ibn Haani´ amesema:

“Wakati mwingine nilikuwa namuona Abu ´Abdillaah (yaani Imaam Ahmad) akiegemea mikono yake pindi anaposimama kwa ajili ya Rak´ah inayofuata na mara nyingine nilikuwa naweza kumuona akikaa kwa kunyooka kisha anainuka.” (Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (01/57))

Maoni haya yako vilevile na Imaam Ishaaq bin Raahuyah ambaye amesema:

“Ilikuwa ndio Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kujisaidia kwa mikono kuinuka pasi na kujali ni mzee au kijana.” (al-Masaa-il (2/147/1) ya al-Marwaziy. Tazama ”al-Irwaa’” (2/82-83))

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 134-135
  • Imechapishwa: 13/08/2017