66. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa tisa wa Aal ´Imraan


al-´Ayyaashiy amesema:

“Ibn Yaziyd amesema: “Nilimuuliza Abul-Hasan kuhusiana na maneno ya Allaah:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja na wala msifarikiane!”[1]

ambapo akajibu: “Kamba ya Allaah ni ´Aliy bin Abiy Twaalib.”

Jaabir ameeleza ya kwamba Abu Ja´far amesema:

“Familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio kamba ya Allaah aliyotuamrisha kushikamana nayo:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

“Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja na wala msifarikiane!”[2]

Baatwiniy huyu na wasapoti wake wanaraddiwa kwa jawabu lililotangulia[3].

[1] 03:103

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/194).

[3] Mlango wa 65

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 104
  • Imechapishwa: 03/04/2017