66. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah – watu wa kati na kati siku zote

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah siku zote wanakuwa kati kwa kati. Kwa ajili hii ndio maana wanasema kuwa Ummah huu uko kati na kati baina ya nyumati zingine na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wako kati na kati baina ya mapote potevu. Inahusiana na haya na mengineyo. Wanamthibitishia Allaah matendo, utashi, matakwa yake, aliyopanga na kukadiria na wakati huohuo wanawathibitishia viumbe matendo, utashi na matakwa yao. Wanafanya hivo kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Hawapingi mipango na makadirio, kama wanavofanya Mu´tazilah, na wala hawapetuki mipaka katika kuthibitisha mipango na makadirio na kumpokonya mja utashi na matakwa yake, kama wanavofanya Jabriyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 153
  • Imechapishwa: 12/01/2024