65. Ndio maana tukatumiliziwa Mitume na kuteremshiwa Vitabu


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Amewatumilizia Mitume ili wawaondoshee hoja.

MAELEZO

Miongoni mwa huruma ya Allaah juu ya waja Wake ni kwamba hakuwaacha wakajichagulia dini juu ya nafsi zao wenyewe. Kutokana na upungufu wao na upungufu wa uelewa wao pengine kile walichokichagua ni shari. Badala ya kuwaacha wakategemea akili yao Allaah (Jalla wa ´Alaa) akawatumilizia Mitume Yake na akawateremshia vitabu Vyake kwa ajili ya kuwabainishia watu ile ´ibaadah anayoitaka kutoka kwao. Kwa ajili ya kuwatakia uongofu na kuwaondoshea hoja akawawekea wazi njia ya kuiendea kheri na njia ya kuiendea shari. Muumini ananufaika na yale Allaah aliyomteremshia. Sambamba na hilo Mitume na Vitabu inakuwa ni hoja dhidi ya kafiri. Kwa hiyo Allaah hakuwaacha waja hivihivi burebure pasi na malengo. Bali amewatumilizia Mitume Yake na akawateremshia Vitabu Vyake na hakuwaacha wakategemea matakwa, akili na fikira zao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 51
  • Imechapishwa: 09/08/2021