65. Makatazo ya muislamu kujifananisha na makafiri

11- Miongoni mwa mambo yanayopelekea katika kuwakufurisha washirikina na makafiri ni maharamisho ya kujifananisha nao katika mavazi yao na mambo ambayo ni maalum kwao. Kujifananisha nao katika ´ibaadah zao ndio khatari zaidi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule ambaye atajifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.”[1]

Kufanya hivi ni katika matawi ya kuwakufurisha na kuwafanya ni maadui. Kwa sababu kujifananisha nao kwa uinje ni dalili inayofahamisha kuwapenda kwa ndani. Lau muislamu ingekuwa kweli anawachukia, basi asingelijifananisha nao.

Ni wajibu kwa waislamu wajifakhari kwa dini yao na wala wasijifananishe na makafiri katika mavazi yao na katika mambo yao maalum. Kubwa na baya kuliko yote ni kujifananisha nao katika dini yao kwa njia ya kwamba tukazua katika dini yetu yanayofanana na zile Bid´ah walizonazo, kama mfano wa mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huku ni kujifananisha na makafiri ambao wanasherehekea mazazi ya al-Masiyh. Sisi hatujifananishi nao katika desturi zao, ´ibaadah zao na mavazi ambayo ni maalum kwao.

[1]  Ameipokea Ahmad (5114) na (5115), Abu Daawuud (4031) na wengineo. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 92
  • Imechapishwa: 21/10/2018