Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Jubayr bin Mutw´im (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Alikuja bedui kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Watu wanaangamia, familia zina njaa na mali zinaagamia. Muombe Mola Wako atunyweshelezee! Hakika sisi tunaomba maombezi kwa Allaah kupitia kwako na kwa maombi yako kwa Allaah.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah ametakasika! Allaah ametakasika!” Hakuacha kusabihi mpaka likajulikana hilo katika nyuso za Maswahabah wake. Kisha akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ole wako! Je, unamjua ni nani Allaah? Hakika Jambo la Allaah ni kubwa zaidi kuliko hivyo. Hakika haombwi Allaah kwa yeyote yule katika viumbe Vyake.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud.

MAELEZO

Mwandishi ametaja mlango huu kwa sababu inahusiana na kuikamilisha Tawhiyd na imani. Yaliyotajwa katika Hadiyth ni miongoni mwa njia zinazopelekea katika shirki, kumuomba Allaah kupitia viumbe. Allaah ni mtukufu zaidi kuliko hivo. Allaah hatakiwi kuombwa kupitia viumbe Wake kwa njia ya kwamba mtu akasema:

“Namuomba Allaah kupitia kwako.”

Lakini mtu anaweza kumuombea mwenzie kupitia viumbe wengine kwa kusema:

“Namuombea fulani kupitia kwako.”

Hili halina neno tofauti na kumuomba Allaah kupitia mtu. Haijuzu, kwa sababu Allaah ni mtukufu zaidi kuliko hivo. Kwani yule aombwaye ni mkubwa kuliko yule mwombezi. Kitu kama hicho hakistahiki kwa sababu Allaah ni mkubwa na mtukufu zaidi kuliko kila kitu. Allaah anatakiwa kuombwa kupitia majina na sifa Zake.

1- Jubayr bin Mutw´im (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Alikuja bedui kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Watu wanaangamia, familia zina njaa na mali zinaagamia. Muombe Mola Wako atunyweshelezee! Hakika sisi tunaomba maombezi kwa Allaah kupitia kwako na kwa maombi yako kwa Allaah.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah ametakasika! Allaah ametakasika!” Hakuacha kusabihi mpaka likajulikana hilo katika nyuso za Maswahabah wake. Kisha akasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ole wako! Je, unamjua ni nani Allaah? Hakika Jambo la Allaah ni kubwa zaidi kuliko hivyo. Hakika haombwi Allaah kwa yeyote yule katika viumbe Vyake.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema “Allaah ametakasika” wakati tunapotokea tukio kubwa, jambo lililompendeza au lililomchukiza, na mambo ambayo yamemshangaza au anayoyakemea. Kuna Hadiyth nyingi juu ya hilo kukiwemo ile Hadiyth kuhusu mkunazi na kwamba Ummah huu nusu ya watu wake watakuwa Peponi.

[1] Abu Daawuud (4726) na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (1547). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (1017).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 180
  • Imechapishwa: 15/11/2018